Breaking

Monday 29 May 2023

TBS YASHIRIKI MAONESHO YA SITA YA MIFUKO NA PROGRAM ZA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI MKOANI KIGOMA

WANANCHI wamehimizwa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na kuhakikisha bidhaa wanazotumia hazijaisha muda wake wa matumizi.

Ushauri huo ulitolewa na Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi wa TBS, Bw.Hamis Seleleko, wakati wa Maonesho ya Sita ya Mifuko na Program za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yaliyofanyika mkoani Kigoma katika viwanja wa Mwanga Community Centre kuanzia Mei 21 hadi 28, mwaka huu.

Mbali na kuhimizwa kutumia bidhaa zilizothibitishwa na shirika hilo, wananchi waliohudhuria maonesho hayo wametahadharishwa kuhusiana na matumizi ya vipodozi vyenye viambata sumu ambavyo vimepigwa marufuku kutumika nchini.

Aidha wananchi waliobahatika kufika kwenye banda la TBS kwenye maonesho hayo, walioneshwa mfano wa vipodozi vyenye viambata sumu ambavyo vimekuwa na madhara ya kiafya kwa watumiaji.

"Wananchi wanapofika kwenye sehemu ambazo vipodozi vyenye viambata vya sumu vinauzwa wasisitize kutoa taarifa TBS, kwani watumiaji ndiyo wanaoathirika zaidi ." Amesema Bw.Seleleko

Pamoja na hayo Bw.Seleleko amesema kupitia maenesho hayo walipata nafasi ya kutoa elimu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kupitia siku maalum iliyoandaliwa kwa ajili yao kwenye maonesho hayo.

" Wajasiriamali walielimishwa kuhusu taratibu za kupata alama ya ubora ya TBS na mpango wa Serikali wa kuthibitisha ubora wa bidhaa kwa wajasiriamali hao bure kwa muda wa miaka mitatu," Amesema

Amesema TBS iliweza kufika kwenye mabanda ya washiriki wa maonesho hayo na kuzungumza nao na wale ambao wamethibitisha bidhaa zao na wale ambao bado ili kujua changamoto wanazokutana nazo na kuwakwamisha kuthibitisha bidhaa zao.

"Lakini tumewapata taarifa kuhusiana na uwepo ofisi za shirika letu katika Kanda ya Magharibi ambayo ipo Kigoma, hivyo wakiwa na shida ni rahisi kufika hapo na kuweza kuhudumiwa," alisema. Afisa Udhibiti Ubora - Mwandamizi (TBS) Bw. Hamisi Simoni Seleleko, akitoa elimu kuhusu masuala ya viwango kwa wananchi na wajasiriamali waliotembelea banda la TBS katika Maonesho ya Sita (6) ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yanayoendelea Mkoani Kigoma .
Mkurugenzi Mkuu (TBS)Dkt. Athuman Y. Ngenya ( wa Pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Meneja wa TBS kanda ya Magharibi Bw. Rodney Alananga (Watatu kushoto) pamoja na maafisa wa TBS alipotembelea maonesho ya 6 ya mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi katika viwanja vya Mwanga Community Center, Kigoma.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages