Watu 15 wamethibitishwa kufariki kufuatia ajali iliyohusisha lori kwenye barabara ya Mityanga-Bukuya nchini Uganda.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Isuzu yenye rangi ya fedha, yenye nambari. UBA 605A, inasafiri kutoka Mji wa Mityana hadi Bukuya ikiwa na wachuuzi wa sokoni.
Uchunguzi wa awali unaonyesha dereva alishindwa kulimudu kabla ya lori hilo kupinduka na kusababisha vifo vya watu 11 papo hapo huku wengine wanne wakifariki dunia walipokuwa wakipatiwa matibabu.
“Dereva ambaye hajafahamika jina lake alishindwa kulidhibiti gari likiwa kwenye mteremko na kusababisha kupinduka na kusababisha vifo vya watu 11 papo hapo na wengine wanne walifia hospitalini na wengine kupata majeraha mabaya na kukimbizwa hospitalini.
15 market vendors die in Kassanda road crashhttps://t.co/RZFayMghom#MonitorUpdates
— Daily Monitor (@DailyMonitor) June 19, 2024
📹Enock Matovu pic.twitter.com/pp0U5P5Vh0
Hospitali ya Mityana na Kituo cha Afya cha Bukuya IV kwa matibabu.
Miili ya marehemu imefikishwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Mityana kwa uchunguzi.
Polisi waliongeza kuwa watu 50 walikimbizwa hospitalini, huku 12 wakiwa katika hali mbaya. Kulingana na mtu aliyeshuhudia, gari hilo lilikuwa limebeba wafanyabiashara zaidi ya 60, na waliojeruhiwa walikuwa wamevunjika mifupa.
"Tuliondoa majeruhi zaidi ya 50, lakini watu 11 walikufa papo hapo. Hii ina maana kwamba lori lilikuwa limebeba watu zaidi ya 60. Majeruhi walikuwa wamevunjika mifupa na walikuwa na maumivu makali wakati tukiwavuta kutoka kwenye mabaki ya lori. " alisema, Isma Ssendagire, shahidi wa macho.