Breaking

Thursday 5 September 2024

WANAWAKE VIONGOZI 37, WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA WA KIMTANDAO


Mkurugenzi Mtendaji wa TAMCODE, Rose Ngunangwa akizungumza wakati Mafunzo ya Ulinzi wa Taarifa na Usalama wa Kimtandao kwa Wanawake Viongozi 37 kutoka mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora. Mafunzo hayo yamefanyika leo Septemba 5, 2024 mkoani Dodoma.

*******************

NA EMANUEL MBATILO , DODOMA

WANAWAKE Viongozi na Vijana wanasiasa wametakiwa kuwa sehemu ya kupunguza hatari za makosa yanayoweza kusababishwa na utumiaji wa mitandao kwa kuhakikisha wanazingatia sheria na miongozo iliyowekwa na Serikali ili umoja, utengamano na staha za watu ziweze kutunzwa na hiyo ni pamoja na taarifa zao binafsi.

Wito huo umetolewa leo Septemba 4,2024 jijini Dodoma na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri wakati akifungua Mafunzo ya Ulinzi wa Taarifa na Usalama wa Kimtandao kwa Wanawake Viongozi 37 kutoka mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora,

Aidha Mhe. Shekimweri alisema usalama na ulinzi katika mitandao ni ajenda muhimu katika kupunguza hatari za makosa yanayoweza kusababishwa na watumiaji wa mitandao.

Alisema mafunzo hayo yamekuja katika kipindi muhimu ambacho Taifa linaelekea katika michakato ya kisiasa na uchaguzi hivyo kujengewa uwezo kwa kundi hilo la vijana na wanawake juu ya matumizi ya simu janja na mitandao ni muhimu kwa kuwa wana nafasi muhimu sana ya kufanya maamuzi kwa ustawi wa Taifa.

Pia alisema ni muhimu kuzingatia sheria na miongozo iliyowekwa na Serikali ili umoja, utengamano na staha za watu ziweze kutunzwa na hiyo ni pamoja na taarifa zao binafsi.

"Idadi kubwa ya watanzania tunatumia mitandao ikiwemo Facebook, Instagram, WhatsApp, Barua pepe, X awali Twitter, Jamii Forums na Blogs nisisitize mazingatio ya sheria kwa ulinzi binafsi kama mtumiaji na kuwalinda wengine." Alisema.

Pamoja na hayo alisema kwa kundi la vijana ni muhimu kujiweka salama zaidi katika mitandao kwa kuzingatia sheria za mitandao ili kujilinda wao binafsi na kuepukana na kuchapisha taarifa zisizohakikiwa, picha zisizo na maadili na zenye kuleta taharuki.

Alisema mafunzo hayo yatawasaidia kuwajengea uwezo wanawake na vijana waliopo katika nafasi mbalimbali za maamuzi na kujifunza namna ya kutunza taarifa, kudhibiti na kukabiliana na ukatili wa Kimtandao na kuhakikisha taarifa binafsi na vifaa vyao vya kazi vinakuwa salama.

Pia alisema suala la ulinzi katika mitandao ni vyema elimu ikiwafikia walengwa mbalimbali kupitia makundi yao kuanzia ngazi za chini za elimu ili kukiandaa kizazi kijacho dhidi ya uhalifu wa mtandao.

Kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa Shekimweri amezitaka taasisi za Umma na asasi za kiraia pamoja na makundi mbalimbali kudumisha amani ili kuendelea kutunza amani ya Taifa na kuwahimiza kujiandikisha katika daftari la kudumu la.wapiga kura.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa YOGE, Adv. Philomena Mwalongo aliwasisitiza viongozi hao kuwa makini na watu ambao wanawatafuta kwaajili ya kupata taarifa zako binafsi.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TAMCODE, Rose Ngunangwa alisema mafunzo hayo yatawafanya viongozi hao kujilinda na matukio ya kiharifu pamoja na kuchafuliwa kwenye mitandao kutokana na uongozi wao.

Akizungumza kuhusiana na mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TAMCODE,) kwa kushirikiana na Taasisi ya YOGE, Miriam Wanjiru kutoka Paradigm Initiative alisema wanawake wapo katika hatari zaidi ya kushambuliwa katika mitandao ya kijamii mara 27 zaidi .

Vilevile kwa upande wake Diwani wa Kata ya Msalato Dodoma Jiji, Nsubi Bukuku alisema mafunzo hayo yatawasaidia katika kujiweka salama zaidi pamoja na kulinda haki zao ikiwemo kujieleza katika mitandao.

"Viongozi tunatakiwa kuwa makini sana kwenye hii mitandao, kwa maana tunaweza kutapeliwa sana, na pia kuweza kuchafuliwa na baadhi ya watu waovu kupitia mitandao ya kijamii ambayo tunatumia na ukizingatia sisi ni viongozi". Alisema
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Ulinzi wa Taarifa na Usalama wa Kimtandao kwa Wanawake Viongozi 37 kutoka mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Ulinzi wa Taarifa na Usalama wa Kimtandao kwa Wanawake Viongozi 37 kutoka mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora. 
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Ulinzi wa Taarifa na Usalama wa Kimtandao kwa Wanawake Viongozi 37 kutoka mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora. .
Mkurugenzi Mtendaji wa YOGE, Adv. Philomena Mwalongo akizungumza wakati Mafunzo ya Ulinzi wa Taarifa na Usalama wa Kimtandao kwa Wanawake Viongozi 37 kutoka mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora. 
Mkurugenzi Mtendaji wa YOGE, Adv. Philomena Mwalongo akisisitiza jambo wakati Mafunzo ya Ulinzi wa Taarifa na Usalama wa Kimtandao kwa Wanawake Viongozi 37 kutoka mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora. 
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMCODE, Rose Ngunangwa akizungumza wakati Mafunzo ya Ulinzi wa Taarifa na Usalama wa Kimtandao kwa Wanawake Viongozi 37 kutoka mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora. 
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMCODE, Rose Ngunangwa akizungumza wakati Mafunzo ya Ulinzi wa Taarifa na Usalama wa Kimtandao kwa Wanawake Viongozi 37 kutoka mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora. 
Miriam Wanjiru kutoka Paradigm Initiative akizungumza wakati Mafunzo ya Ulinzi wa Taarifa na Usalama wa Kimtandao kwa Wanawake Viongozi 37 kutoka mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora. Mafunzo hayo yamefanyika leo Septemba 4, 2024 mkoani Dodoma.
matukio mbalimbali katika picha kwenye Mafunzo ya Ulinzi wa Taarifa na Usalama wa Kimtandao kwa Wanawake Viongozi 37 kutoka mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora. Mafunzo hayo yamefanyika leo Septemba 4, 2024 mkoani Dodoma.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages