Breaking

Sunday 22 May 2022

BABA AKAMATWA TUHUMA ZA KUMLAWITI MTOTO WAKE - ZANZIBAR


Na Samir Salum, Lango la habari

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar linamshikilia Kheir Mkombe Abdallah (39) Mkazi wa Fueni Pangani wilaya ya Magharibi B kwa tuhuma za kumuingilia kinyume na maumbile mtoto wake wa kike (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 11 mwanafunzi wa darasa la tano.

Akithibitisha mbele ya waandishi wa habari leo Jumamosi Mei 21, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi ACP. Abdallah Mussa Amesema Mtuhumiwa huyo alifanya kosa hilo mnamo Mei 10, 2022 majira ya saa Nne usiku huko Fuoni Pangawe na baada ya kufanya tukio hilo mtuhumiwa alimbilia kusikojulikana.

Amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa mnamo Mei 20, 2022 majira ya Saa saba mchana katika Kijiji na Kata ya Likongowele Mkoani wa Lindi.

"Kwa kuwa Jeshi la Polisi lina mkono mrefu limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo kwa kutumia kitengo kinachoshughulikia Makosa ya kimtandao ( Cyber- crime) na kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi" amesema Kamanda Mussa

Aidha Kamanda Mussa ameongeza kuwa taratibu za kisheria zitakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages