Breaking

Wednesday 22 June 2022

WATU WANNE WAFARIKI, 132 WAJERUHIWA AJALI YA TRENI TABORA


Na Lango la Habari

Watu wanne 4 wamefariki dunia na wengine 132 kujeruhiwa baada ya Treni ya abiria iliyokuwa ikitoka Mkoa wa Kigoma kuelekea Mkoani Tabora mpaka Dar es salaam kuanguka katika eneo la Kata ya Malolo iliyopo katika manispaa ya Tabora.

kupitia taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa Shirika la Reli Tanzania Jamila Mbarouk, amesema kuwa kuwa Ajali hiyo imetokea leo Jumatano Juni 22,2022 majira ya saa tano asubuhi ambapo Treni hiyo namba Y 14 yenye injini namba 9019, ikiwa na behewa 8 zilizobeba abiria 930 ambapo Ilipofika eneo la Malolo (Km 10 kutoka stesheni ya Tabora) behewa 5 za abiria daraja la tatu, behewa 1 la vifurushi, behewa 1 la huduma ya chakula na vinywaji na behewa la breki zilianguka na kusababisha ajali.

Bi. Jamila amesema ajali hiyo imesababisha Vifo 4 wakiwemo watoto 2, wakike mwenye umri wa miaka 5 na wakiume miezi 4 na watu wazima wawili, mwanaume na mwanamke na Majeruhi 132 ambapo tayari wamepelekwa katika hospitali ya Mkoa, Kitete - Tabora, kwaajili ya matibabu na wanaendelea vizuri.

Amesema Shirika linaendelea na zoezi la kuwasafirisha manusura wa ajali kutoka Tabora ili kuendelea na safari ya kuelekea Dar es Salaam huku likiendelea kufuatilia kwa karibu, kufahamu chanzo Cha ajali ili kuchukua hatua. 







Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages