Breaking

Wednesday 22 June 2022

MWANAFUNZI WA MIAKA MINNE AFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI LA SHULE - SHINYANGA



Na Samir Salum, Lango la Habari

Mwanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Samuu, Godlight Chisawilo mwenye umri wa miaka minne (04) amefariki dunia baada ya kugongwa na Gari aina ya Toyota Coastar  katika Mtaa wa Majengo Mapya Mkoani Shinyanga.


Akithibitisha hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana Jumanne Juni 21, 2022 majira ya saa 12 jioni ambapo Gari hilo lenye namba za usajili T.151 DAG lilikuwa likitokea Shule ya Awali na Msingi Samuu na kuelekea majengo mapya likiwa limebeba wanafunzi wa shule hiyo akiwemo Godlight.


Kamanda Kyando amesema baada ya kufika Mtaa wa Majengo mapya, Godlight alishuka na kuvuka barabara ambapo dereva wa gari hilo Kassim Said (40) alimgonga na kumsababishia kifo papo hapo.


Kamanda amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kutochukua tahadhali kwa watumiaji wengine wa barabara ambapo tayari amekamatwa na taratibu za kisheria zitafuata.


Aidha ameongeza kuwa Mmiliki wa gari hilo ambaye ni Malatia na Dereva watashitakiwa kwa kupakia wanafunzi katika gari ambalo alama na usajili wa kupakia wanafunzi wa Shule.


Pia ametoa wito kwa madereva kuchukua tahadhari kwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali.


Mwisho

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages