Breaking

Sunday 12 June 2022

RAIA WA CHINA ASAKWA KWA TUHUMA ZA KUUA KWA RISASI KISA MAPENZI - ILALA, DAR



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtafuta Raia wa China Zheng Lingyao (42) kwa tuhuma za kumuua Fu Nannan (26), ambaye pia ni raia wa China, mfanyabishara na mkazi wa Kalenga, Ilala Dar es Salaam.

Akithibitisha hilo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema kuwa tukio limetokea jana jumamosi Juni 11, 2022 saa 5:45 usiku katika mtaa wa Kalenga, Ilala ambapo marehemu alikuwa anaishi kwenye ghorofa ya tatu ya wapangaji.

“Mtuhumiwa anayetafutwa alifika eneo hilo na kumjeruhi kwa risasi tumboni Nie Mnqin (32), raia wa China na badaye alimfyatulia risasi Fu Nannan, raia wa China ambaye alipoteza maisha" amesema Kamanda Muliro 

Ameongeza kuwa Nie anaendelea na matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Aidha, Kamanda Muliro amesema kuwa chunguzi wa awali umebaini kuwepo kwa tatizo la kutoelewana lililotokana na masuala ya kimapenzi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages