Breaking

Sunday 31 July 2022

JAMAA AINGIA MITINI BAADA YA MKEWE KUZAA WATOTO WATANO KWA MPIGO



Jamaa mmoja amezua kioja kwa kuhepa nyumbani kwake baada ya mkewe kujifungua watoto watano kwa mpigo akidai kwamba 'sio jambo la kawaida.

Nalongo Gloria, kutoka Uganda, alitelekezwa na mumewe Ssalongo alipojifungua mtoto wao wa tisa na wa kumi.

Badala ya kutayarisha nyumba yao kwa ajili ya kuwasili kwa ndugu zaidi kwa familia yao inayokua, baba alihepa.

Gloria aliambia NTV Mwasuze Mutya : “Nilipopata ujauzito wa pacha siku ya tatu, mwanamume huyo alisema jambo hili lilimshinda na akaniambia niende nyumbani.

“Huko alikuwa akinituma sikuwa na namba zao tena kwa sababu nilikuja Kampala kufanya kazi ya nyumba.

“Sijutii kuwazaa watoto wote hawa, najua baba yao hapendi, na siwezi kuwaacha popote pale, licha ya changamoto zilizopo, kamwe sitawatelekeza watoto wangu, najua Mungu atanijalia.

“Nimemwachia Maulana maisha yangu. Nimeumia lakini Mola anajua sababu."
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages