Breaking

Saturday 2 July 2022

AJALI YAUA WATU WATANO NA KUJERUHI 17 TABORA



Watu watano wamefariki dunia na wengine 17 kujeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea jana Ijumaa jioni Julai Mosi, 2022 katika kijiji cha Mabangwe wilayani Sikonge mkoani Tabora.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema basi hilo la Sasebosa lilikuwa linatoka mkoani Mbeya kwenda Tabora.

Kamanda Abwao amesema majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa mkoani hapo kwa ajili ya matibabu.


Source: Mwananchi 
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages