Breaking

Sunday 10 July 2022

RAIS, WAZIRI MKUU WAKUBALI KUJIUZULU

Spika wa Bunge la Sri Lanka Mahinda Yapa Abeywardena ametangaza jana kuwa Rais wa nchi hiyo Gotabaya Rajapaksa amekubali kujiuzulu wadhifa wake July 13,2022 kufuatia maandamano ya vurugu.

Tangazo hilo limetolewa baada ya Waandamanaji kumshinikiza Rais na Waziri Mkuu kujiuzulu, Waandamanaji hao walivamia makazi ya Rais na kuchoma moto maakazi ya kibinafsi ya Waziri Mkuu jijini Colombo.

Waziri Mkuu Ranil Wickremesinghe pia amekubali kujiuzulu baada ya viongozi wa vyama kumtaka yeye na Rais aliye madarakani kujiweka kando baada ya nchi hiyo kutumbukia kwenye mdororo wa kiuchumi.

Maandamano nchini humo yamechochewa na mzozo wa kiuchumi ambao haujawahi kutokea na kusababisha uhaba wa mafuta, gesi, dawa na vyakula ambavyo Serikali imeshindwa kununua kutokana na ukosefu wa fedha.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages