Breaking

Saturday 9 July 2022

TANZIA: BI HINDU AFARIKI DUNIA



Msanii mkongwe Nchini Tanzania, Chuma Suleiman almaarufu Bi Hindu ametutoka leo Jumamosi Julai 9, 2022 akiwa Magomeni nyumbani kwake.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na mjukuu wake huku sababu ya kifo chake ikitajwa kuwa ni maradhi ya muda mrefu.

Bi Hindu ni mmoja wa waasisi wa Kaole Sanaa, kundi ambalo lilipata umaarufu mkubwa mwanzoni mwa miaka ya 2000, pia ni mdau mkubwa wa Klabu ya Simba, aliwahi kuonekana mara kadhaa katika matukio yaliyohusu klabu hiyo.

Aidha, amewahi kuwa mmoja wa watangazaji wa Kituo cha E-FM Radio cha Jijini Dar es Salaam.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages