Breaking

Tuesday 16 August 2022

BREAKING: RAILA ODINGA APINGA MATOKEO YA URAIS KENYA



Na Samir Salum, Lango la habari

Mgombea wa Kiti cha Urais wa kenya kupitia tiketi ya chama cha Azimio Umoja, Raila Odinga amepinga matokeo ya Urais yaliyotangazwa jana Na Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC).

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa habari alioufanya leo Jumanne August 16, 2022 katika Ukumbi wa KICC amesema kuwa Mwenyekiti wa Tume huru ya uchaguzi Kenya IEBC Wafura Chebukati ametumia mabavu kutangaza matokeo hayo bila kukubaliana na Makamishna wenzake.

" Chebukati ni Dikteta, amechukuwa madaraka ya tume bila kuhusisha wenzake, Sheria haimruhusu Mwenyekiti wa tume IEBC kutangaza matokeo bila kukubaliana na wajumbe wa tume"

"Takwimu zilizotangazwa na Bw Chebukati ni batili na ni lazima zifutiliwe mbali na mahakama ya sheria."

"Tunakataa kabisa na bila kusita matokeo ya urais yaliyotangazwa jana... Tunafuatilia njia na michakato ya kikatiba na halali ili kubatilisha tamko la Bw. Chebukati haramu na kinyume na katiba" - Raila Odinga


“Mamilioni ya Wakenya walijitokeza kwa wingi katika jaribio la kuchagua viongozi wao... Lakini jana demokrasia yetu chipukizi ilikumbwa na msukosuko mkubwa.

 "Kenya inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kisheria na kisiasa kutokana na hatua ya Wafula Chebukati, mwenyekiti wa IEBC [tume ya uchaguzi].

 "Tulichoona jana ni unyama na kupuuza waziwazi katiba na sheria za Kenya."

Endelea kufuatilia Lango la habari kwa taarifa zaidi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages