Breaking

Tuesday 6 September 2022

KAULI YA RAILA ODINGA BAADA YA UAMUZI WA MAHAKAMA



Na Said Muhibu,LLH

Sekretarieti ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya na Mgombea wa Urais wa Azimio la Umoja Raila Odinga imeshindwa kukubaliana na uamuzi uliofanywa na Mahakama Kuu nchini Kenya baada ya kuidhinisha ushindi wa Urais kwa Naibu Waziri na mgombea wa Urais kupitia chama cha UDA William Ruto.

Taarifa iliyotolewa na sekretarieti hiyo imeeleza kuwa inaheshimu uamuzi uliotolewa na wa mahakama na siku zote imekuwa ikisimamia utawala wa kisheria na katiba, ila hawakubaliani na uamuzi huo.

“Tunaheshimu uamuzi wa Mahakama ijapokuwa hatukubaliani na uamuzi huo,” ilieleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa ushahidi uliotolewa na mawakili wa Raila Odinga ulikuwa ni wa kweli usiopingika huku ikiongeza kwa kuwashukuru wakenya wote walioshiriki katika kupigania haki ya mgombea huyo na kuahidi kudumisha demokrasia, uwajibikaji na uwazi.

Rais mteule William Ruto alitangazwa kuwa mshindi wa kiti cha Urais na Tume ya Uchaguzi na Mipaka Ncini Kenya (IEBC) chini ya Mwenyekiti wake Wafula Chebukati kwa kura asilimia 50.49 akifuatiwa na mpinzani wake Raila Odinga aliyepata asilimia 48.85 mnamo Agosti 15 mwaka huu.

Hata hivyo Raila Odinga aliamua kupinga Uamuzi wa IEBC na kwenda Mahakama kuu Nchini Kenya ili kubatilisha uamuzi huo, jpo la majaji saba likiongozwa na jaji Martha Koome lilihitimisha kusikiliza pingamizi na utetezi kwa pande zote mbili na kutoa uamuzi wa kumuidhinisha William Ruto kuwa Rais wa tano Nchini Kenya.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages