Breaking

Saturday 17 September 2022

RAIS SAMIA KUSHIRIKI MAZISHI YA MALKIA ELIZABETH IIRais Samia amewasili London, Uingereza kwa ajili ya kushiriki shughuli rasmi ya msiba wa Malkia Elizabeth II.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasialiano ya Rais ikulu Zuhura Yunus leo Jumamosi Septemba 17, 2022 imeleza kuwa Siku ya Jumapili, Viongozi mbalimbali walioalikwa akiwemo Rais Samia watatoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu kwenye eneo la Westminster Hall ambapo pia atatia saini kitabu cha maombolezo.

Baada ya hatua hiyo Rais Samia atahudhuria hafla fupi iliyoandaliwa na aliyetamkwa kuwa Mfalme Charles III ambaye amemrithi Mama yake Malkia Elizabeth II.

Siku ya Jumatatu Rais Samia atahuhudhuria mazishi ya Kitaifa ya Malkia II yatakayofanyika kwenye Kanisa la Westminster Abbey, mwili wa Malkia Elizabeth utalazwa kwenye Kasri la Windsor.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages