Breaking

Wednesday 12 October 2022

WANNE MBARONI KWA KUBAKA WATOTO WADOGO, WATATU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA, MMOJA KIFUNGO CHA MAISHA


Na Lango La Habari 

Watu wanne wamefikishwa mahakamani na kukutwa na hatia ya makosa ya vitendo vya Ukatili wa Kijinsia na Unyanyasaji wa Watoto katika Mkoa wa Manyara.

Kupitia Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara ACP George Katabazi ameeleza kuwa watu hao wamefikishwa Mahakamani kutokana na Ushirikiano kati ya Jeshi hilo na Ofisi ya Taifa ya Mashitaka.

Kamanda Katabazi amesema Jumanne Oktoba 10, 2022 watuhumiwa wawili walifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Manyara akiwemo Severine Leonce (25) Mkazi wa Kijiji cha Matufa akituhumiwa kumbaka mtoto wa miaka 14.

Severine alikiri kosa hilo ambapo amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, kuchapwa viboko 12, sita wakati wa kuingia na ÅŸita wa kutoka pamoja na kulipa faini ya Shilingi Milioni Moja.

Mtuhumiwa wa pili ambaye ni Shabani Jumanne (20) Mkazi wa Kijiji cha Magugu naye alihukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 16.

Kamanda Katabazi ameeleza kuwa mnamo Septemba 01, 2022 Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumfikisha Manine Mathayo (20) katika Mahakama ya hakimu mkazi Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara kwa tuhuma za Kumbaka mtoto wa miaka Saba (7).

"Mtuhumiwa alikiri Kosa hivyo alihukumiwa kifungo cha Maisha Jela" ameelezea Kamanda Katabazi

Aidha mnamo tarehe 29.06.2022 katika Mahakama ya hakimu mkazi Wilaya ya Simanjiro mtuhumiwa Justine Ombeni (26) mkazi wa Oljoro alihukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya msingi.

"Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara linaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ili kumaliza vitendo vya kihalifu na unyanyasaji wa kijinsia na Watoto katika Mkoa wetu hivyo niwaombe wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za watu wachache wanajÄ°husÄ°sha na vitendo vya unyanyasaji." Amesisitiza Kamanda Katabazi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages