Breaking

Tuesday 15 November 2022

KISIMA CHA GWAJIMA KUCHANGIA UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI - GOBA



Na Lango la Habari

Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea kuboresha hali ya upatikanaji maji katika Mkoa huo ambao leo imefanya kazi ya kusafisha na kupima ubora wa maji katika kisima cha kwa Gwajima kinachomilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Josephat Gwajima.

Kisima hicho kipo Majengo Salasala, kata ya Goba kikiwa na urefu wa mita 47 na uwezo wa kuzalisha lita 192,000 kwa siku.

Kazi ya uboreshaji wa kisima na kuingiza maji kwenye mfumo wa usambazaji itakamilika 18/11/2022 na kitaingizwa kwenye mfumo rasmi wa usambazaji maji wa DAWASA na kitatumika kuboresha hali ya upatikanaji maji kwa wakazi takribani 1400.



Kutokana na uwepo wa kisima hicho DAWASA inamshukuru Mhe. Gwajima kwa kujitoa na kwa kuchangia katika kuongeza wigo wa upatikanaji maji katika kipindi cha ukame.

Hadi sasa DAWASA inazalisha jumla ya lita milioni 30.3 kwa siku kupitia visima virefu.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages