Breaking

Wednesday 23 November 2022

MAMA ATUHUMIWA KUUA WATOTO WAKE WAWILI KWA MAPANGA




Watoto wawili wenye umri wa miaka kati ya miwili hadi mitano kutoka katika familia moja wameuawa kwa kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao na mtu anayedaiwa kuwa ni mama yao mzazi

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limeanza uchunguzi juu ya tukio hilo

Shan Yohana mama wa watoto hao ndiye anadaiwa kuwaua watoto wake kwenye nyumba wanayoishi, mashuhuda wa tukio hilo wamezungumza.

Akizungumza eneo la tukio, Mkuu wa Oparesheni Mkoa wa Mbeya, Abdi Issango amesema limetokea majira ya saa mbili asubuhi ambapo mazingira ya kifo hicho yanadhaniwa kuwepo kwa mgogoro baina na mama wa marehemu hao na familia yake.

Tayari Jeshi la Polisi limewatia nguvu mama wa marehemu hao Shan Yohana, mdogo wake pamoja na mtoto aliyesalimika kwenye tukio kwa ajili ya hatua za kisheria na matitabu kwa majeruhi.

Via: EATV
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages