Breaking

Friday, 11 November 2022

RAIS SAMIA AZINDUA MRADI WA MAJI KIGAMBONI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakivuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa Mradi wa maji Kigamboni ambao unatoa maji lita milioni 70 kwa siku kwa ajili ya wakazi wa maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia maji baada ya kuwasha mtambo (pampu) wa kutoa maji chini ya ardhi kwenye kisima kirefu (m 450) kwa ajili ya kuyapeleka kwenda kwenye tanki kubwa la maji katika eneo la Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuwasha mtambo (pampu) wa kusukuma maji kwenye tanki kubwa la maji kwa ajili ya usambazaji kwa wakazi wa maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusiana na mradi mkubwa wa maji ya visima 7 ambao unatoa maji zaidi ya lita milioni 70 kwa siku kwenye hafla iliyofanyika Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuzindua Mradi wa maji Kigamboni ambao unatoa maji lita milioni 70 kwa siku kwa ajili ya wakazi wa maeneo mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam kwenye hafla iliyofanyika Kigamboni tarehe 11 Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso pamoja na viongozi mbalimbali wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi na ugawaji wa magari ya mitambo kwa ajili ya kuchimbia visima virefu na mabwawa sehemu mbalimbali nchini kwenye hafla iliyofanyika Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mfano wa ufunguo, Waziri wa Maji Jumaa Aweso pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga mara baada ya kuzindua na kugawa magari ya kuchimbia visima virefu na mabwawa sehemu mbalimbali nchini kwenye hafla iliyofanyika Kigamboni Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wananchi kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa maji Kigamboni ambao unatoa lita milioni 70 za maji kwa siku kwa ajili ya wakazi wa maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam 11 Novemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Viongozi pamoja na Wananchi baada ya kuzungumza nao kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa maji Kigamboni ambao unatoa lita milioni 70 za maji kwa siku kwa ajili ya wakazi wa maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam 11 Novemba, 2022.
Wananchi wa Kigamboni pamoja na maeneo jirani wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Kigamboni ambao unatoa maji lita milioni 70 kwa siku kwa ajili ya wakazi wa maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2022.

*********
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inakwenda kutekeleza ujenzi wa bwawa la maji la Kidunda mkoani Morogoro litakalotumika kukusanya maji wakati wa mvua.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais ikulu Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais Samia amesema hayo leo wakati akizundua miradi ya maji Kigamboni, kukabidhi mitambo ya kuchimba visima na ujenzi wa mabwawa pamoja na kukabidhi eneo la ardhi kwa mkandarasi wa mradi wa bwawa la maji la Kidunda.

Aidha, Rais Samia amesema bwawa hilo lenye thamani ya shilingi bilioni 329 litakalojengwa kwa kutumia fedha za ndani litawezesha kuwepo uhakika wa maji kwa kipindi cha mwaka mzima jijini Dar es Salaam na maeneo ya mkoa wa Pwani ambayo kwa sasa yanategemea maji ya Mto Ruvu.

Ujenzi wa bwawa hilo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka huu 2022 mpaka 2025 ambapo utakapokamilika utachochea kasi ya maendeleo ya viwanda katika mkoa wa Pwani pamoja na Dar es Salaam.

Kwa upande mwingine, mradi wa maji wa Kigamboni utaimarisha huduma ya maji katika maeneo ya Temeke, Ilala na Kinondoni hivyo kupunguza ukali wa mgao wa maji.

Hali kadhalika, Rais Samia ameiagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuhakikisha inasambaza maji kwa wananchi katika wilaya ya Kigamboni kwa asilimia 100.

Rais Samia ameitaka Wizara ya Maji kutoa elimu kwa wananchi kuacha kuchoma misitu ovyo, kuchepua maji pamoja na kuingiza mifugo hasa wananchi wanaoishi kando ya vyanzo vya maji kwani vitendo hivyo husababisha upungufu wa maji.

Pages