Breaking

Wednesday 9 November 2022

WAFUKUA KABURI NA KUNYOFOA ULIMI, JICHO NA MOYO WA MAREHEMU

Picha haihusiani na tukio



Watu wasiojulikana wamefukua mwili wa mwanamke Neema Mlomba mwenye umri wa miaka 26 na kunyofoa baadhi ya viungo vyake ikiwemo moyo katika Kijiji cha Luteba Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera, ameagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa haraka kuwabaini watu waliohusika na hilo

Homera amesema mbali na moyo viungo vingine vilivyonyofolewa ni Ulimi na jicho la kulia huku tukio hilo likihusishwa na imani za kishirikina.

Mtoto wa marehemu wa Neema yuko hospitali ya Wazazi Meta chini ya uangalizi maalum wa madaktari akiendelea kupatiwa huduma za matibabu.

Via EATV
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages