Breaking

Tuesday 15 November 2022

WATU 11 WAKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA AKIWEMO KOCHA WA MAKIPA SIMBA SC




Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) inawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya huku miongoni mwao akiwemo Kocha wa Makipa wa Klabu ya Simba, Muharami Mohamed ‘Shilton’.

Kupitia taarifa iliyitolewa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Gerald Kusaya leo Jumanne Novemba 15, 2022 amesema kuwa Mamlaka hiyo iliendesha Operesheni katika maeneo mbali mbali ya nchini na kukamata Jumla ya Kilo 34.89 za dawa za kulevya aina heroin.

Katika watuhumiwa hao 11 waliokamatwa yumo Mfanyabishara na Mmiliki wa Kituo cha Michezo cha Cambiasso Sports Academy, Kambi Zubeir Seif.

Amesema watuhumiwa wengine ni Seleman Matola (24) mkulima na mtoto wa dada yake na mtuhumiwa Seif, Said Matwiko (41) fundi seremala, Maulid Mzungu (54) ambaye anaundugu wa mtuhumiwa Sultan ambaye ni kocha wa Simba.

“Wengine waliokamatwa ni John Andrew (40) mkazi wa Magore Kitunda, huyu ni mfanyabiashara pia ana jukumu la kutafuta vijana wenye vipaji na kuwapeleka kituo cha Cambiasso Sports Academy, Rajabu Dhahabu (32) mfanyabiashara na mkazi wa Tabata Segerea, Hussein Pazi (41) pamoja na Ramadhan Chalamila (27)” alisema Kusaya

Kusaya alisema katika tukio jingine mamlaka hiyo ilimkamata mtuhumiwa Abdulnasir Kombo (30) ambaye ni mkazi wa Kaloleni jijini Arusha akiwa na biskuti 50 zilizotengenezwa kwa kutumia dawa ya kulevya aina ya bangi kama moja ya malighafi aliyokuwa akiiuza katika eneo la Jiji hilo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages