Breaking

Sunday 13 November 2022

WAZIRI MCHENGERWA AWATAKA MA'RC KUHAMASISHA MICHEZO


Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini kuhamasisha shughuli za michezo na sanaa ili kuibua vipaji na kuimarisha afya zao.

Waziri Mchengerwa ametoa wito huo leo Jumamosi Novemba 12, 2022 Usiku kwenye hotuba yake ya kufunga mashindano ya Kikapu, kombe la CRDB jijini Tanga.



Amesema kwa upande wa Serikali, tayari imepanga kukarabati viwanja saba ikiwa ni maandalizi ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON 2027.

" Tunatamani kuona kila wilaya kuwe na kiwanja na kwa kufanya hivyo mtakuwa mnatekeleza Sera ya Utamaduni." Amefafanua Mhe. Mchengerwa



Aidha ametoa wito kwa Halmashauri zote nchini kutenga maeneo na fedha kwa ajili ya kujenga viwanja vya kisiasa vya michezo.

Amewataka kuandaa Mpango wa kazi ili kuona ni namna gani Wizara inavyoweza kusaidia utekelezaji wake.

Awali Waziri Mchengerwa alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano, Samia Suluhu Hassan kwa maono yake na hamasa kubwa anazozitoa kwenye Sekta za michezo hali ambayo imesaidia kuleta mafanikio makubwa katika kipindi kifupi cha utawala wake.



Ameyataja baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni pamoja na timu za soka za Serengeti Girls na Tembo Warriors kufuzu robo fainali Kombe la Dunia, Kuwa mwenyeji wa mashindano ya dunia ya Mr na Miss Death nakushinda.

Mengine ni wachezaji 10 wa Tembo kusajiliwa vilabu vya kimataifa barani ulaya wakati wachezaji sita wa Serengeti Girls wamepata nafasi ya majaribio Marekani.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages