Breaking

Wednesday 21 December 2022

RAIS AFUTA NYOGEZA YA MSHAHARA WA MWISHO WA MWAKARais wa Msumbiji Filipe Nyusi mnamo Jumanne alifuta malipo ya nyogeza ya mwezi Desemba kwa watumishi wa umma walio na kandarasi, na hivyo kumaliza mtindo wa kila mwaka ambapo wafanyakazi wa serikali mara nyingi walipata marupurupu ya ziada mwishoni mwa mwaka.

Katika hotuba yake bungeni, Rais Nyusi alitaja changamoto kali za kiuchumi lakini akasema wafanyakazi wote wanaolipwa pensheni watapokea malipo yao ya ziada ambayo yanajulikana kama 'mshahara wa 13'.
Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni iliyodumu kwa saa mbili, Rais Nyusi aliliambia bunge katika hotuba ya kila mwaka ya hali ya taifa kwamba nchi inakabiliwa na mzigo ambao Ngazi ya Mshahara Mmoja (TSU) iliunda katika azma ya kudhibiti matumizi ya kawaida ya umma.

TSU bado haijatekelezwa lakini bunge limeanza mijadala ya kuhalalisha sera hiyo ambayo inastahili kuondoa malipo ya mishahara na marupurupu mengine.

Chanzo: The East africa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages