Breaking

Thursday 15 December 2022

SERIKALI YAOMBWA KUANZISHA MAKUMBUSHO YA BIBI TITINa John Mapepele

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeiomba Serikali kuanzisha makumbusho ya Bibi Titi ili yatumike Kwa ajili ya kurithisha mchango na maono yake ya harakati za kupigania uhuru wa Tanzania Kwa vizazi vya sasa.

Akitoa mada ya Siasa na Uongozi kwenye Kongamano la Tamasha la Bibi Titi Mohamed Ikwiriri-Rufiji leo Desemba 15, 2022 Profesa, Shani Omary kutoka UDSM amesema Bibi Titi ana historia kubwa inayopaswa kutuzwa.Tamasha hili limeratibiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye pia ni Waziri mwenye dhamana ya Utamaduni, Sanaa na Michezo hapa nchini.

Aidha, amesisitiza kuwa kituo hicho cha makumbusho kinatakiwa kujengwa Rufiji ambapo kitakuwa kivutia cha kizuri cha utalii wa Utamaduni.


Naye Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda na waMkoa wa Pwani bi Zainabu Vulu kwa nyakati tofauti wameiomba Serikali kuanzisha taasisi maalum ambayo itakayohusika na Bibi Titi Mohamed kama ilivyo kigoda cha Mwalimu Nyerere kwa upande wa wanaume.

Aidha, wameiomba Serikali kuwa na siku maalum kwa ajili ya kuadhimisha siku ya Bibi Titi huku wakisisitiza kuandikwa kwa kitabu kinachomwelezea kiongozi huyu shupavu, mwanaharakati na mpigania uhuru wa Tanzania.Tamasha hili limeanza Jana na linaendelea jioni ambapo wasanii mbalimbali watatoa burudani kutoka Zanzibar na Tanzania Bara.

Katika Tamasha hili ambalo Mhe. Chatanda alikuwa Mgeni Rasmi lilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul, Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi Wabunge, na viongozi mbalimbali kutoa maeneo mengine.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages