Breaking

Tuesday 6 December 2022

SERIKALI YAPONGEZWA KUJENGA CHUO CHA VETA KARAGWE



Na Richard Mrusha Karagwe

Mkuu wa Chuo cha ufundi (VETA )Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera Pascal Thomas amesema kuwa chuo hicho ni miongoni mwa vyuo vya Veta katika wilaya ya Karagwe,na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeamua kuwekeza katika vyuo vya ufundi na ikapanua huduma zake katika vyuo vya wilaya ambapo hapo awali kulikuwa na vyuo vya mkoa na vyuo ambavyo vilikuwa kwenye kanda tu

Amesema kuwa wao karagwe wapo kanda ya ziwa ambayo inaunganisha mikoa ifuatayo Mwanza ,Mara ,kagera pamoja na Geita na katika mkoa wa kagera ambao una wilaya zifuatazo karagwe Misenyi ,kyerwa ,Ngara ,Muleba ,Biharamuro pamoja na Bukoba hivyo katika vyuo ambavyo vimepandishwa hadhi ni pamoja na chuo cha karagwe ambapo chuo hicho kihistoria kilianza mwaka 1986 na kilikuwa kinamilikiwa na mtu binafsi ambaye alikuwa anaitwa Edmin Mkenda ambaye kwasasa ni Marehemu.


Thomas ameyasema haya Disemba 5,2022 wilayani karagwe wakati akizungumza na waandishi wa Habari waliofika chuoni hapo.

amesema kuwa baada ya aliyekuwa mmiliki wa chuo hicho kuona gharama za uendeshaji zinakuwa kubwa ndipo aliamua kukabidhi kwa Halmashauri ya wilaya hiyo tangu mwaka 1992 na kuanzia mwaka huo chini ya Halmashauri ya wilaya kiliendelea kutoa huduma ya mafunzo ya ufundi nchini hivyo mpaka sasa hivi kinaendeshwa na Serikali kwa asilimia mia moja.

“Tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyowezesha Chuo cha Veta wilayani karagwe ,chuo cha Veta karagwe kinauwezo wa kupokea vijana 250 kwa kozi ndefu lakini hata hivyo kinazo kozi fupi fupi ambazo zinaendeshwa chuoni hapo

na zaidi ya vijana 450 ambao tunaweza kuwapokea kwa mwaka hivyo uwezo wake hadi hivi sasa ukiweka kozi ndefu na fupi inamaana karibu vijana 700 wanaweza kupokelewa na mpaka sasa tunao vijana 250 ambao wanategemea kufanya mtihani wa taifa ambao wa mwaka wa kwanza na mwaka wa pili.”amesema Thomas

Ameongeza kuwa wanaishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuweza kuwa fadhili vija wasio nauwezo wa kifedha wapatao 109 ambao wanafadhiliwa kusoma kwa kozi mbalimbali ya miezi sita na sasa hivi wanakwenda kuhitimu kozi hiyo na vijana hao wamekuwa wakiwafundisha kwa muda wa jioni hivyo mpaka sasa hivi wanakwenda kuhitimu.

Amesema Serikali imeweza kutoa shilingi bilioni 4.6 71 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa chuo hicho na pia ameweza kutoa shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kununua vifaa na mitambo katika kalakana hivyo sasa hivi kalakana zimekamilika kwa asilimia kubwa.

Na Kwa upande wake mwanafunzi wa chuo hicho David Adam ambaye anasoma kozi ya muda mfupi ( DMO) ambayo imedhaniwa na ofisi ya Waziri mkuu na mafunzo yao yameanza Juni sita mwaka huu na wanamalizi Disemba 12 mwaka uhu na kozi hiyo ililenga mafunzo ya ufundi stadi wa kozi mbalimbali ikiwamo Umeme.Selemala, Fundi magari .Uwashi., na ujenzi hivyo wanatoa shukrani kama watanzania ofisi ya Waziri mkuu kwa kudhamini mafunzo hayo kwani wengine walikuwa hawana uwezo wa kugharamia mafunzo hayo.

Naye Mwanafunzi Mwingine Raines Oscar Amesema kuwa yeye anasoma kozi ya Ukutubi kwa mda wa miaka miwili na nusu hivyo wanampongeza nje Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya na Mwenyezi MUNGU ambariki sana kwani anachokifanya anakwenda kugusa Maisha ya watanzania masikini
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages