Breaking

Saturday 10 December 2022

WANANCHI KARAGWE WANUFAIKA UUZAJI WA ZAO LA KAHAWA KWA MNADA, DC BINYURA AISHUKURU SERIKALI



Na Richard Mrusha Karagwe

MKUU wa Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera Mwalimu Julieth Binyura amesema wilaya ya yake ina kata 23 na vijiji 77 na wananchi wa wilaya hiyo ni wakulima ,wafanyakazi na wafugaji nakwamba katika shughuli za kilimo wananchi wanalima kilimo cha mazao ya migomba ,mahindi,maharage., viazi mviringo pamoja na alizeti wanalima kwa wingi na maendeleo ya wananchi yanategemea kilimo na ufugaji.

Amesema kwaupande wa kilimo wanajitahidi sana kulima hasa mazao ya biashara hususani zao la kahawa ambapo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameweza kuwaletea mfumo wa uuzaji wa kahawa kwanjia ya mnada ambapo wakulima hao walipokea kwa upendo mzuri na wameweza kuuza vizuri kulingana na mnada ambao umepita na kila mmoja amepata haki yake na walipokuwa wakiuza walikuwa wanapata fedha zao baada ya siku moja pasipokuwa na mgogoro wowote.

Mwalimu Julieth alisema hayo Desemba 8 mwaka huu wilayani humo wakati alipokuwa akizungumza na vyombo mbalimbali vya Habari ofisini kwake ambapo amesema kuwa wananchi hao wanaendelea kumuombea Rais Dkt Samia kwa kuweza kusababishia kupanda kwa bei ya kilo ya zao la kahawa na kumefanya wauze shilingi 2800 kwa kilo moja hadi 3000 hivyo wamefurahia bei hiyo nzuri.

Ameongeza kuwa kwa upande wa mifugo kwenye wilaya ya Karagwe wanafuga kisasa na kutumia fursa ya vyombo vya Habari kuwatangazia wananchi kuwa kuja kujifunza kwa mwekezaji anayeitwa Kahama Freshi nakwamba yeye ni mfugaji ana mifugo yake inayofugwa kitalaamu kwani ukienda kwake anakuelekeza vizuri unafundishwa vizuri hivyo wanawakaribisha wananchi wote Kwenda kujifunza.

na Kwaupande wake Kaimu Meneja Mkuu wa Chama kikuu cha Ushirika (KDCU LTD), Domitian Kigunia alisema kuwa kuna vyama vya msingi 140 ambavyo vinawakulima wanachama zaidi ya 64,000 na majukumu yao kama chama kikuu cha ushirika ambacho ndio mwamvuli wa vyama vya msingi ni kuhakikisha vyama hivyo vinapata huduma stahiki ambapo chini yake kuna wakulima.

Alisema kuwa wajibu wa Chama hicho nikuhakikisha wanapata masoko kwa ajili ya wakulima wao lakini pia kutoa huduma zinazolenga kuleta tija katika uzalishaji kwahuduma ya ugani na kuwajengea uwezo wakulima hao ili kuzalisha kwa tija .

“Tunaendelea na majukumu yetu kwa maana ya kuhakikisha mkulima anapata tija ya kutosha na kama chama kikuu chenye wanachama 140 tunahakikisha tunatoa huduma ambazo zina,muwezesha mkulima kuzalisha kwa tija ,huduma kama ambavyo kimsingi tunatekeleza nikuhakikisha tunakuwa na maofisa ugani na wanawahudumia wakulima na wanatoa elimu ya kilimo ili kuweza kuzalisha kwa tija na katika hilo chama kimeajili maafisa ugani 23na wapo vijiini na kazi yao na muda wao unatumika katika kuwajengea uwezo wakulima ili waweze kuzalisha kwa tija”amesema

Amesema kuwa kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali na wanadau walioako nje ya nchi wanahakikisha kwamba wanapata soko la mazao hasa ambalo wanalisimamia ni zao la kahawa na kimsingi kwa mwaka huu wakulima wameweza kupata faida kutokana na maboresho yaliyofanyika kupitia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutaka kahawa iuzwe kwa njia ya mnada.

Kwaupande wa baadhi ya wakulima wa zao la kahawa wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa Habari waliotembelea kwenye mashamba yao wamemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea mfumo wa mauzo kwa njia ya mnada hatua ambayo imewafanya kuweza kupata faida na kunufaika na zao hilo huku wengine wakieleza wamefanikiwa kujenga nyumba,kusomesha Watoto,na kununua usafiri.

Alexsander Andrea mkulima wa zao la Vanila alisema anamiaka mitatu kwenye kilimo hicho ambapo alishauriwa na wenzake kujikita kwenye kilimo hicho cha Vanila na anamshukuru Mbunge wa Jimbo hilo la Karagwe Innocent Bashungwa kwa kuweza kumuunga mkono lakini pia rais Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa kilimo Hussein Bashe ambao kwa pamoja wamemsaida hapo alipofikia hususani kwenye zao la Vanila.

Naye James fundulo alisema yeye anajishughulisha na kilimo cha migomba na ,maharagwe,mtama,na kwamba anamshukuru Rais kwa kuleta mfumo wa kuuza mazao yao hususani zao la kahawa kwamaana hivi sasa wanauza kwa mara moja na kupata faida kubwa ambapo kwa sasa inawasaidia kuendesha Maisha yao ukilinganisha na siku za nyuma ambapo walikuwa hawana uhakika na soko na kujikuta wakipunjwa.

Alisema kuwa katika kilimo anachofanya faida kubwa anaiona kwenye zao la kahawa na rais amefanya jambo kubwa sana na ameweza kuwakomboa kupitia mauzo kwa njia ya m nada,na licha ya kilimo lakini pia wanamshukuru Rais Dkt Samia kwa wao kama wazee kuweza kupata matibabu bure na wanapata dawa kikamilifu lakini pia wanamshukuru Mbunge wao Innocent Bashungwa kwa kuweza kutilia mkazo.




Mwisho.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages