Breaking

Tuesday 27 December 2022

WATANO WAFARIKI AJALI YA GARI MOROGORO



Watu watano wamefariki dunia papo hapo, katika eneo la Mikumi, wilayani Kilosa mkoani Morogoro katika ajali iliyohusisha gari ndogo maarufu kama IT iliyokuwa ikitokea bandarini jijini Dar es salaam kuelekea mpakani Tunduma kugongana uso kwa uso na gari kubwa la kusafirisha mafuta lilokuwa likitokea mkoani Iringa kuelekea mkoani Morogoro.

Akithibitisha kutokea Kwa ajali hiyo, Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Morogoro Fortunatus Musilimu amesema ajali hiyo imetokea majira ya usiku wa kuamkia jumatatu eneo la Iyovi wilayani Kilosa barabara kuu ya Morogoro - Iringa na kuongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva aliyekuwa akiendesha gari ndogo aliyefahamika kwa jina la Festo Shoo ambaye alikuwa katika mwendo kasi na kutaka kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake bila kuangalia kwa makini mbele yake.

Kamanda Musilimu amesema waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni watu watano wanaume wanne na mwanamke mmoja ambao wote walikuwa katika gari dogo (IT).


Chanzo: matukioDaima
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages