Breaking

Wednesday 1 February 2023

RAIS SAMIA AITAKA MAHAKAMA KUIMARISHA MIFUMO YA UTOAJI HAKI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi Mbalimbali pamoja na Majaji kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma


Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiwa kwenye Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma kwa ajili ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria Tanzania


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Hamis Juma pamoja na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu mara baada ya kuhutubia kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria Tanzania yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Hamis Juma mara baada ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria Tanzania yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Hamis Juma pamoja na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mahakama mara baada ya kuhutubia kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria Tanzania yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma

……………………………..

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kushirikiana na Wizara za kisekta kuzifanyia marekebisho sheria zote zenye mizunguko inayochelewesha kesi na upatikanaji wa haki.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais ikulu Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais Samia ametoa agizo hilo leo Jumatano Februari 01, 2023 katika maadhimisho ya Siku ya Sheria yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali.

Aisha, Rais Samia amesema Sheria mbalimbali zimetoa nafasi ya usuluhishi katika Mabaraza ya Vijiji na Kata hivyo amewataka majaji na Mahakimu kutoa mafunzo kwa kutumia utaratibu wa usuluhishi wa migogoro.

Rais Samia amewaagiza wadau wote katika Sekta ya Sheria kupitia upya taratibu ambazo mashauri hupitia ili kuzifupisha kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa haraka.

Vile vile, Rais Samia amesema anatarajia kuona Watanzania wanatambua kwamba kufikishana mahakamani sio jambo la lazima na badala yake usuluhishi iwe ndio njia ya kwanza kutumika.

Rais Samia pia amesema ni lazima mfumo wa utoaji haki unaochukua muda mrefu kutatua migogoro urekebishwe kwa kuwa ni hatari, huongeza gharama na kuathiri mazingira ya uwekezaji na biashara.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ameitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwachukulia hatua watumishi ambao wanachafua sura na taswira ya muhimili wa Mahakama kwa vitendo viovu vya rushwa, kauli mbaya na hata vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake, watoto na wenye uhitaji maalum.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages