Breaking

Tuesday 7 February 2023

TETEMEKO LINGINE LAIPIGA UTURUKI, VIFO VYAFIKIA 5000 TETEMEKO LA ARDHI UTURUKI, SYRIA



Idadi ya vifo inaongezeka hadi sasa zaidi ya 5,000 vimerekodiwa kutokana na tetemeko lilitokea siku ya jumatatu.

Nchini Uturuki, idadi ya watu ambao wamekufa kwa sababu ya matetemeko haya ya ardhi imeongezeka hadi 3,381, kulingana na mamlaka ya maafa nchini humo.

Orhan Tatar, afisa katika Mamlaka ya Usimamizi wa Maafa na Dharura (AFAD), anasema wengine 20,426 wamejeruhiwa na majengo 5,775 yameporomoka.

Hesabu hiyo mpya inafikisha idadi ya waliofariki nchini Uturuki na nchi jirani ya Syria kufikia 4,890. Idadi hii huenda ikazidi kuongezeka.



Tetemeko jipya la ardhi lenye nguvu limeripotiwa katikati mwa Uturuki.

Utafiti wa Jiolojia kutoka Marekani unasema tetemeko lenye ukubwa wa 5.5 lilikuwa katika kina cha kilomita 10 (maili 6) karibu na mji wa Golbasi.

Wakati huo huo, Kituo cha Ulaya-Mediterranean Seismological Center (EMSC) chenye makao yake nchini Ufaransa kiliweka nguvu ya tetemeko kuwa karibu na Golbasi 5.6, na kuongeza kuwa lilikuwa katika kina cha 2km.

Mashirika yote mawili yalisema tetemeko hilo lilitokea saa 03:13 GMT siku ya Jumanne. Hawakutoa maelezo zaidi.

Eneo la Kusini-mashariki mwa Uturuki limekumbwa na mfululizo wa mitetemeko kufuatia tetemeko kuu la ardhi karibu na mji wa Gaziantep Jumatatu asubuhi.

endelea kuwa nasi kwa matukio yote ya hivi punde.


Via: BBC

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages