Breaking

Saturday, 25 March 2023

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI, ACHAPWA VIBOKO HADHARANIWakazi wa kijiji cha Kibwera wilayani Geita mkoani Geita nchini Tanzania wamemuadhibu mwanamume mmoja kwa kuvuka mipaka ya maadili. 


Mwanamume huyo aliyetambulika kwa jina la Katayo Bote alinaswa na mke wa mtu mwingine wakirushana roho hali iliyowakasirisha wakazi wa eneo hilo. 


Katayo alipigwa viboko hadharani na kutozwa faini ya shilingi Laki mbili kufuatia kisa hicho kilichowaudhi wenyeji. Emmanuel Ndalawa aliyeumia moyoni alisema alimfumania Katayo akimtafuna mke wake mdogo chumbani kwake, kama ilivyoelezwa na Millard Ayo.


 Ndalawa alisema kwa siku nyingi, aligundua mpenzi wake alikua akionesha upendo usio wa kawaida kwake Katayo tangu walipohamia eneo hilo. 


Ndalawa ambaye ana wake wawili, alisema alimkuta mke wake wa pili na mdogo akijivinjari na Katayo, landilodi wa chumba walichopangisha. 
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages