Breaking

Wednesday 19 July 2023

PAROKO AUAWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO - KARATU



Paroko wa Kanisa la Katoliki, Parokia ya Karatu mkoani Arusha, Pamphili Nada ameuwa kwa kupigwa na kitu kizito na mtu anayedaiwa kuwa na afya ya akili aliyeingia Kanisani kwa nguvu kutaka kusali.

Hata hivyo baada ya mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Romani Leonard (30) kufanya mauwaji hayo naye ameuawa na Wananchi wenye hasira.

Kamanda wa polisi mkoa Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo leo Jumatano Julai 19, 2023.

"Padri alifariki wakati anapelekwa hospitali na mtuhumiwa aliuawa na wananchi wenye hasira baada ya kupata taarifa za tukio hilo,"amesema.

Soma zaidi >>hapa<<

Chanzo: Mwananchi

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages