Breaking

Wednesday 30 August 2023

MABALOZI WA TANZANIA NJE YA NCHI KUIBEBA SEKTA YA MADINI



Leo Agosti 30, 2023 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo amewapokea Waheshimiwa Mabalozi Wapya walioteuliwa hivi karibuni kuiwakilisha Tanzania nchini Canada, Namibia, Austria, Oman na Ufaransa jijini Dodoma.

Ziara hiyo ya Mabalozi imelenga kufahamishwa kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini nchini.

Katika kikao hicho Mabalozi watapata taarifa kutoka katika taasisi za Wizara ya Madini, Tume ya Madini, Taasisi za Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), STAMICO, TEITI na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC).

Mabalozi hao waliotembelea Wizara ya Madini ni Balozi Joseph Sokoine anayekwenda Canada, Balozi Fatma Rajab- anayekwenda Oman, Balozi Naimi Azizi- anayekwenda Austria, Balozi Ali Jabir Mwadini - anayekwenda Ufaransa na Balozi Ceaser Waitara -anayekwenda Namibia
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages