Breaking

Thursday 28 September 2023

WAJUMBE WA KAMATI ZA ELIMU NA AFYA ZAIPONGEZA TGNP KWA KUWAPATIA MAFUNZO

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WAJUMBE wa Kamati za Elimu na Afya wameushukuru Mtandao wa Jinsia Tanzania kuwapatia Mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya jinsia katika majukumu yao.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Sept 27,2023,Mjumbe wa bodi ya Afya Amos Hangaya Kabisi,ameishukuru Taasisi ya TGNP,kwa kuwapatia elimu ya kupanga bajeti yenye mlengo wakijinsia.

"kwa sababu kulikuwa Mambo tunayatekeleza tukiamini watu wote wako sawa,lakini kumbe kuna makundi inatakiwa kuyatazama kwa jicho la pili,lakini katika utekelezaji wa maisha ya kawaida kumbe Kuna mtu yawezekana alishindwa kufika kliniki kwa sababu ya kukosa uwezo au elimu,hivyo tunatakiwa kutoa elimu na huduma kwa mlengo wa kijinsia ili kupunguza vifo vya mama na mtoto"Amesema

Aidha Bw.Amos amesema Bodi na kamati zote zilizo pata elimu hiyo zikipewa uwezo ndani ya mwaka huu au mwaka ujao kutakua na mabadiriko makubwa kwa bodi na kamati ndio watendaji wakuu katika upatikanaji wa huduma za kila siku.

Kwa Upande wake Mjumbe wa Kamati ya shule Mwl.Grace Kifwembe kutoka shule ya msingi Majohe amesema amejifunza kuhusu mfumo dume ambao unaanzia majumbani.

"Tulikua tukiamini unakuta mtoto wakike ni mdogo tunamlazimisha afanye kazi aoshe vyombo afue nguo za Kaka tukidhani Ni haki mtoto wa kiume asifanye kazi kumbe huu mfumo hautakiwi mtoto wa kiume na wa kike wapewe kazi sawa na kupata muda wa kumpumzika kwa Pamoja"Amesema

Pamoja na hayo amesema watoto wa kike wanamahitaji yao maalumu tofauti na watoto wa kiume ambayo yanatokana na hali ya kimaumbile.

"Kwamba tunapokua na watoto wa kike shuleni tunatakiwa kuwapa kipaumbele,kila shule ina vyoo,je ni kweli mtoto wa kike shuleni Ana chumba maalumu kwa ajiri ya kujisitiri anapokumbwa na Ile hali?je napale shuleni kamati ya Afya Ina akiba ya taulo za kike kwa ajili ya kujisitiri anapokumbwa na Ile hali?"Amesema

Semina hiyo ya Wanakamati wa Afya na Elimu iliyo beba dhana ya usawa wa kijinsia imefikia tamati siku ya Jumatano.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages