Breaking

Sunday 3 September 2023

WATUMISHI WA TBS WAKUTANA PAMOJA KWENYE VIWANGO SPORTS BONANZA

 NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limeshiriki Bonanza la Michezo kwa wafanyakazi wa shirika hilo lengo likiwa ni kuwakutanisha pamoja watumishi katika michezo ili kuboresha afya na kujenga mahusiano mazuri.

Akizungumza hapo jana Septemba 2,2023 katika Bonanza hilo ambalo limefanyika kwenye viwanja vya Gwambina Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya TBS, Prof.Othuman Chande  amewapongeza wanaviwango waliojitokeza kushiriki pamoja na kushangilia katika kipindi chote cha bonanza.

“Hii itasaidia kuboresha afya zao na kujenga mahusiano mazuri kati ya watumishi, kwani utekelezaji mzuri wa majukumu yenu ya kila siku hutegemea sana afya ya mwili na akili”. Amesema

Amesema watumishi na watoa huduma wa Shirika la Viwango Tanzania wameshiriki katika michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, mpira wa Pete, mpira wa wavu, kuvuta kamba na michezo ya jadi ambapo mashindano haya yameshindanishwa kiidara.

“Vilevile kupitia michezo hii watumishi hupata burudani na hupunguza msongo wa mawazo unaoweza kusababishwa na kukosa nafasi ya kufanya mazoezi au kushiriki michezo mbalimbali”. Amesema


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages