Breaking

Wednesday 18 October 2023

AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KULAWITI WANAWAKE WATATU



Na Jeshi La Polisi

Mahakamani ya Hakimu mkazi Wilaya ya Njombe Oktoba 17,2023 imemhukumu kifungo Cha miaka 30 Jela Juma Radsalaus Msemwa miaka 27, Mkulima na mkazi wa Kihesa kosa la kuwabaka wanawake watatu huko mtaa wa Kihesa kwa kuwafungia ndani na Kisha kutekeleza tukio hilo

Akisoma hukumu hiyo ya kesi CC No 53/2023 Hakimu mkazi wa Wilaya ya Njombe Mhe. Matrida Kayombo amesema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo 30 Mei 2023 huko Kihesa wilaya ya Njombe kabla ya kufikishwa na Mahakamani na kupatikana na hatia.

Aidha mshitakiwa alisomewa mashita yote sita na kupatikana na hatia kwa Makosa yote sita ambapo mtuhumiwa amefungwa miaka 30 kwa Kila kosa na kufanya jumla ya 180 ambapo adhabu hiyo itakwenda kwa pamoja Ili iwe fundisho kwa wengine.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages