Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Mhe. Mobhare Matinyi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali.
Kupitia taarifa iliyotolewa leo Jumapili Oktoba 01, 2023 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus imeeleza kuwa Kabla ya uteuzi huo Bw. Matinyi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.
Uteuzi huu unaanza mara moja