Breaking

Wednesday 11 October 2023

TGNP YAPONGEZWA KATIKA HARAKATI ZA KUMKOMBOA MTOTO WA KIKE KIFIKRA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KATIKA Kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, Mtandao wa Jinsia Tanzania imekuwa mstari wa mbela katika kuhakikisha watoa mafunzo jinsi ya kuendelea kumlinda mtoto wa kike dhidi ya ukatili kwenye jamii na maeneo mengine yanayomzunguka.

TGNP imekuwa na Kampeni za mara kwa mara kuhakikisha mwanamke anapata haki zake zote za msingi, na miongoni mwa kampeni ambazo wamkuwa wakizifanya ni pamoja na kampeni ya kupinga ukukutaji kwa watoto wa kike, kampeni ambayo ilibeba kauli mbiu "HAKEKETWI MTU ilikuwa ni kipinndi ambacho mtoto wa kike anapelekwa kwenye Mila za ukeketaji.

Akizungumza leo Oktoba 11,2023 katika Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS), Mwanaharakati Bi.Zawadi Kondo amesema katika kuhakikisha mwanamke anakomboka kifikra, wameangazia jitihada mbalimbali katika kuendelea kumlinda mtoto wa kike na kumjengea uwezo katika masuala ya Uongozi.

"Tumeona vitu mbalimbali TGNP wamefanya kama kuanzisha vilabu vya jinsia mashuleni ambavyo vimekua chachi katika malezi ya mtoto na vile wanavyo fundishwa na walimu ambao ni walezi wao"Amesema

Aidha Bi. Zawadi ameipongeza TGNP katika jitihada zao katika urekebishwaji au Ushauri wa Sera ambazo zinatengenezwa na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha jamii inaishi kwa usawa na kupata haki zote za msingi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages