Breaking

Wednesday 1 November 2023

HABARI NJEMA KWA WAKAZI WA MAKABE HADI KIBULULU

Habari njema kwa wakazi wote wa maeneo ya Makabe, Tegeta A, Mbezi, Makongo Juu, Goba, Changanyikeni na Kibululu kuwa ofisi ya DAWASA MAKONGO inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi.

Zoezi hili linaenda sambamba na utoaji wa elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano na malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.

Takribani wateja zaidi ya 150 wa maeneo hayo wanatarajia kuanza kunufaika na huduma ya majisafi.

Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0736602601 (DAWASA Makongo).

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages