Breaking

Tuesday, 14 November 2023

KAMATI YA BUNGE YAJIONEA MAANDALIZI YA MASHAMBA YA MBEGU MAMA

  

Na Nyabaganga Taraba - Arusha

Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania imeendelea na ziara yake ya kutembelea miradi ya Wizara ya Kilimo kwa kutembelea baadhi ya miradi iliyoko mkoa wa Arusha

Ikiwa mkoani Arusha Novemba 13,2023 imetembelea miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji ya taasisi za TARI na Wakala wa uzalishaji Mbegu Tanzania (ASA) na kujionea maandalizi ya mashamba ya uzalishaji Mbegu mama kwa upande wa taasisi ya utafiti(TARI) na mashamba ya uzalishaji mbegu kwa ajili ya wakulima yaliyo chini ya Wakala wa Mbegu Tanzania (ASA) yaliyoko eneo la Ngalamtoni na Tengeru na TARI Seliani.


Mwenyekiti wa Kamati hiyo Daniel Sillo amesema hawana shaka na kazi zinazoendelea katika mradi hiyo 

Wakichangia na kutoa maoni yao wanakamati hao wamewataka TARI na ASA kuhakikisha wanatoa elimu kwa umma kuhusu kazi na huduma wanazotoa zinawafikia wananchi .

Wakati wa hitimisho la ziara Mkurugenzi wa ASA Dk Sophia Kashenge amewapitisha wanakamati kwenye wasilisho lenye takwimu za hali ya sekta ya kilimo ilivyo kwa sasa takwimu zote ni nzuri kwa mipango ya nchi ila takwimu iliyoonyesha ongezeko la ukuaji wa kilimo kuwa ni 3.4 asilimia na ongezeko la watu hapa nchini kuwa ni 3.2 asilimia ni kuwa karibu sawa ni changamoto ambayo inahitaji hatua za kuitatua kama taifa ili kuepuka upungufu wa chakula kwani hii ni ishara kuwa tunakoelekea kama hatutachukua hatua za uzalishaji tutajikuta tuko kwenye uhitaji mkubwa wa chakula siku za uso ni jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa chakula.

"Changamoto hii inatuhimiza kuongeza juhudi katika sekta hii kama taifa na kama mtu mmoja mmoja hususani vijana ni vyema wajikite katika sekta hii wazee wakulima wamepungua takwimu zinaonesha",amesema.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages