Breaking

Tuesday 28 November 2023

TTB YAONGOZA WATALII 165 KUTEMBELEA HIFADHI YA MIKUMI

Bodi ya Utalii Tanzania kupitia Mradi wa REGROW leo tarehe 27/11/ 2023 imeongoza watalii 165 wa umoja wa watu wenye usikuvu hafifu kutoka nchi 40 ambapo wamepata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

Vivutio vya Utalii vya Tanzania vina miundombinu rafiki inayowawezesha watu wenye mahitaji maalum kuvimbelea na kufurahia uzuri wa vivutio vya Utalii vya asili vya Tanzania.

Wakiwa hapa nchini wameweza kufanya kongamano pamoja na kuendesha Mashindano ya Ulimbwende na Utanashati Miss & Mister Deaf International 2023 ambayo yamefanyika tarehe 25/11/2023 jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania , Robert Masunya ambaye ni kiongozi wa Msafara, akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa shindano la ulimbwende na utanashati.
Baadhi ya wajumbe wa happy Deaf Family waliyotembelea Hifadhi ya Mikumi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages