Breaking

Friday 17 November 2023

WATATU WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA KWA KOSA LA MAUAJI


Na Jeshi la Polisi

Mahakama Kuu Kanda ya Iringa ambayo imewahukumu watu watatu kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kuua kwa kukusudia na wawili miaka mitatu kwa kosa la kushiriki katika mauaji.

Watuhumiwa hao, Zawadi Fabain Mlowe ambaye alihukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kuua kwa kukusudia, alitenda tukio hilo mwaka 2016 kesi Na MC 97/2016. Hukumu hiyo imetolewa mbele ya Jaji Mhe. A. E. Mwaipopo.

Pili, Batoni Mangula Baraka amehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kuua kwa kukusudia watu wawili, alitenda tukio hilo mwaka 2017 kesi Na 41/2019. Hukumu hiyo imetolewa mbele ya Jaji Mhe. A. A. Mrisha.

Tatu, Joel Joseph Nziku amehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa kuua kwa kukusudia watoto watatu mtuhumiwa alitenda tukio hilo mwaka 2019 kesi Na MC 108/2022. Hukumu hiyo imetolewa mbele ya jaji Mhe. A.A Mrisha.

Wengine wawili ni Lusitika Hussein Nguvila na Obiko Lifed Ngogo hawa walifungwa miaka 3 kwa kushiriki katika kosa la Mauaji, walishiriki kutenda kosa hilo mwaka 2023 kesi MC 54/2023 hukumu hiyo imetolewa mbele ya Jaji Mhe. A. A. Mrisha.

Wakisoma hukumu hizo majaji kwa nyakati tofauti wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa inayofanya vikao vyake Njombe wamesema watuhumiwa hao wote walitenda makosa hayo katika maeneo tofauti hivyo Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote kwamba watuhumiwa hao walitenda makosa hayo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages