Breaking

Thursday 16 November 2023

WATOTO WATANO WAFARIKI WAKIDHANIWA KULA CHAKULA CHENYE SUMU


Watoto watano wa familia moja wamefariki dunia katika kijiji cha Nyakanazi Wilaya ya Biharamlo mkoani Kagera kwa kile kinachosadikika kula chakula chenye sumu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema kuwa vimetokea kwa nyakati tofauti baada ya wanafamilia 11 kula chakula cha usiku Novemba 13, 2023.

Chatanda amesema, wanafamilia hao baada ya kula chakula cha usiku walienda kupumzika lakini asubuhi yake watoto watatu Brayan Ezekiel (2), Kahindi Samson (9) ambaye ni mwanafunzi wa awali shule ya msingi Muungano na Happines Razaro (12) mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Muungano walianza kujisikia vibaya wakakimbizwa kituo cha afya Nyakanazi wakati wanaendelea na matibabu Novemba 14, 2023 wakapoteza maisha.

Wawili waliofariki ni Melisiana Razaro (11) na Melina Razaro (9) huku Josephina Juma (5) akiendelea na matibabu katika hospitali hiyo.../

Soma zaidi >>HAPA<<

Via: Mwananchi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages