Breaking

Monday 19 February 2024

UDSM YAFANIKIWA KUSAJILI JARIDA LA "AFRICAN REVIEW"

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam, Ndaki ya Sayansi za Jamii, kimafanikiwa kufanya usajili wa Jarida lake la pili ambalo limepewa jina la "African Review"kwenye faharasa ya kanzi data ya Scoopers ambayo huwa inaonesha majarida ya Kimataifa yanayofanya vizuri.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 19 2024,Katika Hafla fupi ya kuujulisha Umma mafanikio hayo, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- Utafiti, Prof. Nelson Boniface amesema kuwa ni ndoto ya chuo Kikuu Cha Dar es kuingiza majarida yake yote 24 katika kanzi data kubwa ili yaonekane duniani kote.

Amesema kuwa lengo la machapisho hayo nikuonesha ubora wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kimataifa na wafanyakazi wake kutambulika.

Aidha Prof. Boniphace amesema kuwa Kuna majarida ya ndani ambayo hayajasajiriwa na kanzi data kubwa zilizoko Ulimwenguni ambapo ameeleza kuwa kunajuhudi zinazofanywa kupeleka machapisho hayo katika kanzi data zinazotambulika kimataifa kwa lengo la kujenga muonekano.

"Ukienda kwenye kanzi data zkama Google Scholar utaona wafanyakazi wetu wanaonekana huko,ukienda kwenye kanzi data nyingine ambazo sio kubwa sana Dunia inataka ikuone kupitia hizo na sisi kwa kutambua udhaifu huo kwa mwaka 2022 tulikua machapisho 1200 ambayo yalikua katika majarida ya yetu ya ndani juhudi zetu ni kuyapeleka huko"Prof.Boniphace amesema

Kwa Upande wake,Prof.Christine Noe amempongeza Mhariri Mkuu kwa mafanikio hayo ambayo yanakua kielelezo Cha umataifishaji wa Tafiti zinazofanyika nchini,ambapo itakuwa fursa kwa Ndaki nyingine kufanya hivyo.

Nae,Mhariri Muendeshaji wa Jarida la African Review Dkt.Rodrick Henry amesema sababu za kurudishwa majarida mengine ni muundo wake kutoka oana na Muundo wa Jarida hilo na mbinu za utafiti ambazo hazioneshi kuwa sawia na Jarida.

"Kukataliwa ni Jambo la kawaida kwa sababu ni Jambo la kitaaluma unaweza kukuta Jarida haliendani na dhima Jarida mfano unaweza kukuta ni Jarida linaongelea mambo ya Siasa, maendeleo unaweza kukuta mtu ameleta kitu tofauti kabisa,kingine ni muundo wa Jarida,mbinu za utafiti unakuta mbinu haziendani na kile kitakiwa na jarida"amesema Dkt.Henry

Aidha Dkt Henry amesema kuwa wanautaratibu wakuboresha miongozo Mara kwa Mara kwa ajili ya kupata makala Bora za kiwango Cha juu Cha kisayansi ambapo itawasaidia kubaki katika kiwango Cha Juu na kubaki katika kiwango Cha kitaasisi kisichobadirika.

Ndaki ya Sayansi za Jamii adhima yao kuu ni kufikisha Tafiti zinazofanyika nchini katika anga za kimataifa kwa lengo la kugusa maisha ya watu kutokana na tafiti zinazofanywa na wataalamu wa Sayansi za Jamii nchini,na kukuza jina la taasisi husika na kutambulika mchango wa wataalamu hao Ulimwenguni.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages