Breaking

Monday, 5 February 2024

WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUNADI KAZI ZA VIONGOZI WANAWAKE

Washiriki wa kikao kazi wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Na Rose Ngunangwa - Dar es salaam

Waandishi wa habari wameaswa kunadi kazi nzuri zinazofanywa na viongozi wanawake nchiini ili kuwawezesha wananchi kujua umuhimu wa kuwachagua wanawake kwenye chaguzi.

Wito huu umetolewa leo Februari 5,2024 na madiwani wanawake katika jiji la Dar es Salaam wakati wa kikao kazi cha siku moja kilichoandaliwa na shirika la POLLICY jijini Dar es Salaam chini ya mradi wa VOTE: WOMEN, mradi wa uongozi unaotumia zana za kidijitali kwa wanawake kufuata matamanio yao ya uongozi wa kiraia.

Akichangia katika majadiliano hayo, Diwani wa Segerea Mheshimiwa Lucy Lugome amesisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kunadi kwanza kazi za viongozi wanawake waliopo madarakani ili kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia ambao hufanywa wakati wa chaguzi.

Awali akifungua kikao hicho, Rachel Magege Mratibu wa Mradi huo wa VOTE:WOMEN kutoka POLLICY ameeleza kuwa lengo la mradi huo ni kuwajengea uwezo wa kidijiti viongozi wanawake.

“ Mradi huu pia unafanya kazi na viongozi wanawake Uganda na Senegal na tumeonelea ni vema tukawakutanisha viongozi wanawake na waandishi kwani ni muhimu kazi zao zikaonekana kwa wananchi. Tungetamani kuona mafanikio zaidi ya wanawake viongozi yakiandikwa na kutangazwa na vyombo vya habari,” alisema Magege.

Kikao hiki kinakuja huku watanzania wakijiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa.



Mratibu wa Mradi POLLICY Najma Matengo akizungumza 

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages