Breaking

Saturday 29 June 2024

KAMPUNI YA GEM & ROCK VENTURE YAPONGEZWA KUFANYA MNADA WA MADINI



WADAU wa madini wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wamempongeza Mkurugenzi wa kampuni ya GEM & Rock Venture, Joel Saitoti kwa kufanya mnada wa madini kwenye eneo hilo hivyo kuwanufaisha kiuchumi.

Kampuni ya GEM & Rock imeendesha mnada wa kuuza madini ya Tanzanite kwa wachuuzi wenye leseni kwenye kituo cha Tanzanite Magufuli, ndani ya ukuta unaozunguka migodi hiyo, ambapo wamemshukuru Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Joel Saitoti.

Mdau wa Madini ya Tanzanite Mirerani Boaz Ambonya amesema kampuni ya GEM & Rock ya Joel Saitoti imefanya jambo jema kuendesha mnada wa Madini ya Tanzanite kwani imeongeza wigo mpana wa uchumi wa mji mdogo wa Mirerani.

“Hakika tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu minada kama hii kufanyika na tunampongeza Saitoti kwa kuendesha mnada huu ambao utawanyanyua wajasiriamali wengi kiuchumi,” amezema Vicky Kessy

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages