Breaking

Friday 25 February 2022

ZAIDI YA WATU 130 WAUAWA, 300 WAJERUHIWA VITA YA URUSI NA UKRAINE







Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine amesema kuwa, Zaidi ya watu 137 wameuawa katika siku ya kwanza tu ya vita vya Russia nchini mwake.

Shirika la habari la AFP limemnukuu Zelenskyy akisema hayo mapema leo Ijumaa Februari 25, 2022 na kuongeza kuwa, tangu vilipoanza vita vya pande zote za Russia dhidi ya nchi yake, zaidi ya watu 137 wameshauawa na 306 wamejeruhiwa katika kipindi cha chini ya masaa 24 yaliyopita.

Vile vile amelalamika kuwa nchi za Magharibi za Ulaya na Marekani zimeiacha mkono nchi yake na hivi sasa Ukraine iko peke yake katika kukabiliana na Russia.

Rais huyo wa Ukraine ametoa mwito kwa wananchi wa nchi hiyo wajilinde wenyewe na wasitarajie msaada wa kijeshi kutoka nchi za Magharibi.

Jumatatu ya tarehe 21 Februari, Russia ilitangaza kutambua uhuru wa majimbo mawili ya Donetsk na Luhansk katika eneo la Donbas, mashariki mwa Ukraine baada ya nchi za Magharibi kutojali usalama wa kitaifa wa Russia.

Jana Alkhamisi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ilisema kuwa, imeamua kuanzisha operesheni maalumu ya kijeshi nchini Ukraine ili kuzuia kutokea vita vikubwa vya dunia.

Aidha akizungumza na televisheni ya "Rusia 24," Rais Vladimir Putin wa Russia amesema, lengo la nchi yake si kuliangamiza jeshi la Ukraine bali ni kudhooofisha uwezo wa kijeshi wa nchi hiyo na kuhakikisha kuwa usalama wa Russia unalindwa kwa kuyazuia madola ya Magharibi na NATO kukusanya majeshi yao katika mipaka ya Russia.

Endelea kufuatilia Lango la habari kwa taarifa zaidi 
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages