Breaking

Friday 11 March 2022

"AFRIKA KUTUMIA SARAFU MOJA ITAIMARISHA UCHUMI" - WAZIRI NALEDI



Afrika Kusini imesema inaunga mkono wazo la kuanzisha sarafu moja ambayo itaimarisha miamala ya kibiashara miongoni mwa nchi za bara hilo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini Naledi Pandor, kama nchi hiyo ilivyofanywa katika majukwaa na mikutano mbalimbali ya Afrika, itaendelea kuunga mkono Mkataba wa Abuja wa mwaka 1991, unaotaka nchi za bara Afrika zitangamane na ziondokane na vizingiti na vikwazo vya kibiashara.

"Kuundwa Benki Kuu ya Afrika (ACB), Benki ya Uwekezaji Afrika (AIB) na Shirika la Fedha la Afrika (AMI) ni suala muhimu ambalo litafanikisha mchakato wa kuanzisha sarafu moja ya Afrika, itakayoimarisha biashara miongoni mwa nchi za bara hili."  Naledi amesisitiza

Waziri  Naledi ameongeza kuwa, kuzinduliwa rasmi Eneo la Biashara Huru la Afrika (AfCFTA) mnamo Januari Mosi 2021, ilikuwa hatua kubwa katika kujumuisha soko la pamoja la nchi za Afrika. Mpango huo unatazamiwa kuongeza biashara kati ya mataifa ya Afrika kutoka 18% hadi 50% ifikapo mwaka 2030.

Mwaka jana Jumuiya ya Uchumi ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS ilipasisha ramani mpya ya njia ya uzinduzi wa sarafu moja mwaka 2027, baada ya mpango wa awali wa kuzindua sarafu hiyo kuvurugwa na janga la Corona.

Nchi wanachama wa ECOWAS zinatarajia kuwa, matumizi ya sarafu hiyo iliyopewa jina la 'Eco' yatapiga jeki biashara na ustawi wa chumi za nchi hizo za Magharibi mwa Afrika.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages