Breaking

Friday 11 March 2022

VITA YA URUSI NA UKRAINE KUATHIRI ZAIDI UCHUMI WA MATAIFA YA AFRIKA - IMF




Mkuu wa shirika la fedha duniani IMF, Kristalina Georgieva, amekutana na mawaziri wa fedha wa mataifa ya Afrika kujadili athari za uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

Katika Mkutano uliofanyika jana Ijumaa Machi 10, 2022Kristalina amesema mtazamo wa kiuchumi wa Afrika uko katika hatari ya kupanda kwa bei ya vyakula na mafuta kutokana na vita hivyo.

Mataifa ya Afrika pia yanaathiriwa na kupungua kwa mapato yatokanayo ya utalii na kupungua kwa upatikanaji wa huduma za kifedha.

Ameongeza kuwa nchi nyingi zitalazimika kurekebisha sera zake, na kuongeza kuwa IMF iko tayari kuzisaidia nchi za Afrika kupunguza gharama za marekebisho yoyote ya kisera.

Vita nchini Ukraine tayari vinapandisha bei ya ngano, na kusababisha hofu ya kutokea uhaba wa chakula huku nchi hizo zikiwa viara wakubwa wa uuzaji wa nafaka nje.

Bei ya mafuta pia inapanda, na hivyo kusababisha mzigo kwa chumi dhaifu za mataifa ya Afrika.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages