Breaking

Sunday 20 March 2022

BASATA YATANGAZA WASANII WATAKAOWANIA TUZO ZA MUZIKI TANZANIA, WCB HAWAMO

Mfano wa Tuzo





Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limetangaza  majina ya wasanii walioteuliwa kuwania tuzo za muziki ambapo wasanii kutoka lebo ya wasafi hawapo.

Orodha hiyo imetolewa leo Jumamosi Machi 19, 2022 na Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Matiko Mniko na katika orodha hiyo haina msanii hata mmoja kutoka lebo ya Wasafi huku sababu ikielezwa kuwa hawakupeleka kazi zao wakati wa kukusanya ambapo wasanii 1360 ndio waliopeleka. TAZAMA ORODHA CHINI

Hata hivyo mnamo Machi 14, 2022 katika kipindi cha the switch cha wasafi Fm wakati CEO wa WCB wasafi Nasib Abdul Maarufu Diamond Platnumz akihojiwa alisema kuwa suala la tuzo za muziki Tanzania ni zuri ila hayuko tayari kushiriki.

Alisema kuwa sababu ni kuwa anataka kushiriki tuzo za kimataifa ili alete heshima nchini huku akidai kuwa kama WCB ikishiriki tuzo zote wanaweza kuchukua wao.



TAZAMA HAPA CHINI WASANII WALIOCHAGULIWA KATIKA VIPENGELE VYA TUZO ZA MUZIKI TANZANIA













Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages