Breaking

Thursday 24 March 2022

MAITI YAOKOTWA MTO RUHUJI, NJOMBE




Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Njombe kwa kushirikiana na wananchi mkoani hapa wamefanikiwa kuopoa mwili wa mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50 kwenye maji ya Mto Ruhuji ambaye hajafahamika ni mkazi wa eneo gani, mwili wake ukiwa umenasa kwenye mawe ya mto huo.

Tukio hilo limetokea kwenye mto eneo la njiapanda ya barabara kuu ya kuingia mjini Njombe na njia panda ya barabara ya kutoka Njombe kwenda wilayani Makete.

Akizungumza mara baada ya askari wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani Njombe wakishirikiana na wananchi kufanikiwa kuutoa mwili wa mtu huyo, Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Inspector Loth Madauda amesema kuwa bando chazo hakijajulilana kutokana na mazingira ya eneo husika.

“Mazingira ya eneo ni sehemu ya maporomoko ya maji ambapo alinasa chini ya mawe kwa hiyo inaonekana kama ni mtu aliyetoka kwenye mto mwingine kwa hiyo hatujui chanzo chake katokea wapi.”

Vile vile Inspector Loth Madauda ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na maji yanayotiririka.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages