Breaking

Sunday 20 March 2022

MREMA ATANGAZA KUOA, " NIMEPATA BINTI MDOGO MWEUPE"





Mwenyekiti wa TLP Taifa, Augustino Mrema ametangaza kufunga ndoa siku ya Alhamisi Machi 24, 2022 katika Parokia ya Uwomboni kijijini kwake Kiraracha Mkoani Kilimanjaro.


Mrema mwenye umri wa miaka 77 aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi ya Parole Nchini anafunga ndoa hiyo mara baada ya kumpoteza mke wake Rose Mrema aliyefariki Dunia mwaka jana.


Mrema amesema amepata "binti mwenye umri mdogo" mweupe ambaye ni chaguo lake na watafunga pingu za maisha baada ya kufuata taratibu zote za kikanisa pamoja na ulipaji wa mahari.


Amesema kilicho msukuma kuoa ni kumpata msaidizi wa maisha yake kwani yeye ni mzee na anahitaji mtu wa karibu wa kumwangalia na kumsaidia kwa ukaribu huku akiishukuru familia yake kwa kumkubalia.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages